Watoto wenye wazazi 3 kuzaliwa karibuni

...................

Inawezekana kuzalisha mtoto wazazi watatu
Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa inawezekana kwa wao kuwazalisha watoto kutoka kwa wazazi watatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Wanasayansi hao wanasema kuwa wanasubiri mabadiliko katika sheria na badiliko katika mtazamo ya watu kabla hawajapandikiza manii kwa mayai kutoka kwa wanawake wawili .
Madaktari hao wa uzazi wanasema kuwa wanaweza kuzalisha watoto wenye siha nzuri iwapo wataruhusiwa kisheria kuondoa magonjwa kutoka kwenye chembechembe za uzazi na kupandikiza mbegu za kiume kutoka kwa baba mzazi.
Hata hivyo mipango hiyo tayari imevutia tahadhari kutoka kwa halmashauri inayosimamia utabibu wa uzazi nchini Uingereza.
Inawezekana kuzalisha mtoto wazazi watatu
Huku ikibainika kuwa kunahaja ya mbegu za uzazi kusafishwa na zile zenye maradhi kuchujwa kitaalamu bila ya kupoteza uwezo wa mama kumzaa mtoto asiye na maradhi ya kurithi.
Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kati ya watoto 6500 wanaozaliwa kuna mmoja aliyeambukizwa maradhi kutoka kwa wazazi wake kupitia celi zijulikanazo kama (mitochondria.) ambazo zinasababisha maradhi kama kukosa nguvu mwilini kupofuka maradhi ya moyo na hata wengine hufa.
Watafiti na madaktari wa maswala ya uzazi chini ya nembo ya Human Fertilisation and Embryology Authority (HFEA)waliohudhuria kongamano hilo walishuhudia hatua kwa hatua jinsi utaalamu huu unaweza kumsaidia mama ambaye anaseli za mwili zilizoambukizwa akisaidiwa kumzaa mtoto bila ya maradhi hayo kwa usaidizi wa mwanamke mwenye seli nadhifu na yenye afya.
Inawezekana kuzalisha mtoto wazazi watatu
Prof Andy Greenfield alisema hawana hakika iwapo utalamu huu ni salama kutumika kwa binadamu hadi pale mtoto atazaliwa baada ya kutimika kwa teknolojia hii mpya.
Serikali kwa upande wake imeipungia teknolojia hii kwani itaisaidia jamii kutoathirika na magonjwa ambayo hurithishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Daktari mkuu , Prof Dame Sally Davies, akisema ni jambo la dharura ambalo serikali inasubiri tu kuafiki utafiti huo na kisha kupitisha sheria zitakazoruhusu watoto wenye wazazi watatu

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: