"Mchawi" akataliwa kuingia Dubai
Mwanamume wa Ujerumani ambaye
anaongoza rikodi ya dunia kuwa na mwili uliotogwa mara nyingi kabisa
ameketaliwa ruhusa ya kuingia Dubai, baada ya kwenda huko kutokeza
katika klabu ya starehe.
Rolf Buchholz, ametogwa mwahala 453 kwenye mwili na uso wake na ana pembe mbili kwenye kipaji.Ameeleza kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikataliwa na maafisa wa uwanja wa ndege kuingia nchini kwa sababu, kama alivosema, alikuwa "mchawi".
Bwana Buchholz ameapa kuwa hatarudi tena Falme za Kiarabu.
chanzo:bbcswahili
0 comments: