Match Preview- Yanga- Simba, Mtoto hatumwi dukani jumamosi hii.
KLABU kongwe za Yanga na Simba zinakutana kwa mara ya kwanza Jumamosi hii ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania bara iliyoanza kutimua vumbi Septemba 20.
Timu hizo zenye ushindani mkubwa zinakutana zikiwa katika nafasi tofauti kwenye msimamo wa ligi hiyo unaoongozwa na Mtibwa Sugar mabingwa wa mwaka 1999 na 2000.
Yanga ambao ndiyo wenyeji katika mchezo huo wa Jumamosi ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizo cheza msimu hiyo inatokana na baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya vinara Mtibwa Sugar.
Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na hali mbaya baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi tatu ilizocheza msimu huu na zote kuambulia sare na kujikuta ikiwa nafasi ya 10 na pointi zao 3.
Kuelekea kwenye mpambano huo presha imezidi kupanda kwa mashabiki wa timu zote mbili ambazo mara mechi yao ya mwisho kukutana zilitoka sare ya kufungana bao 1-1,lakini matokeo ya mechi za hivi karibuni yanaipa nafasi ya kufanya vizuri Simba ambayo imeanza vibaya msimu huu.
Simba imeweza kutoka sare na timu za Coastal Union,Polisi Moro na timu ngeni katika ligi ya msimu huu Stand United kibaya zaidi ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa taifa Dar es Salaam
Simba inaingia katika mchezo huo tegemeo pekee likiwa kwa kmshambuliaji wake raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye amekuwa na mchango mkubwa tangu asajiliwe msimu huu akitokea kwa mahasimu wao Yanga.
Ingawa Okwi hakwenda kwenye kambi ya Afrika ya Kusini lakini kocha Patrick Phiri,anatarajia msaada mkubwa kutoka kwa Mganda huyo sambamba na winga Ramadhani Singano na mkongwe Amri Kiemba ambaye Jumapili iliyopita alionyesha kiwango cha juu na kufunga bao la pili katika ushindi wa 4-1 kati ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Benin.
Faraja nyingine ya kocha Phiri ni kureja uwanjani kwa kipa wake chaguo la kwanza Ivo Mapunda aliyekuwa ameumia kidole cha mkono lakini mshambuliaji mpya Raphael Kiongera na nahodha wa zamani Nassor Masoud Chollo watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeruhi yanayo wakabili
Tofauti na Yanga ambao kikosi chao kina na ari kubwa ya kupata ushindi niwazi kitakuwa na lengo la kutaka ushindi katika mechi hiyo ili kuwafikia Mtibwa Sugar katika uongozi wa Ligi hiyo.
Kocha Marcio Maximo amekuwa na matumaini makubwa katika pambano hilo ambalo kwakwe litakuwa la kwanza tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo mwezi Julai mwanzoni
Niwazi Maximo atakuwa akitaka kujiwekea rekodi ya kuifunga Simba na kupata ushindi wa tatu mfulilizo kwenye mechi za Ligi Kuu kwa sababu idadi kubwa ya wachezaji wake waliokuwa wagonjwa wamepona na wapotayari kwa mchezo huo wa leo.
Maximo kwenye sehemu ya ulinzi atakuwa anategemea zaidi ulinzi wa Nadiri Haroub ‘Cannavaro’Kelvini Yondani huku Oscar Joshua aliyekosa mechi mbili zilizopita kutokana na maumivu ya paja aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Mtibwa akitarajia kumtumia baada ya kupona na kuonyesha kiwango cha juu kwenye mechi ya Taifa Satrs dhidi ya Benin Jumapili iliyopita.
Na katika safu ya ushambuliaji Yanga itakuwa ikiwategemea zaidi wachezaji Geilson Santana JAJA,Hamisi Kiiza Andrey Coutinho na Nizar Khalfani huku safu ya kiungo ikiwategemea zaidi Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Hassani Dilunga ambaye ambao wamekuwa kwenye kiwango cha juu siku za karibuni.
Kwa kikosi hiki niwazi Maximo atataka vijana wake wacheze kandanda safi ili kushinda na kufuta uteja wa kufungwa na Simba kwani rekodi zinaonyesha katika miaka mitano timu hizo zimekutana mara 11 simba imeshinda mara nn Yanga mara tatu na mara nne zimetoka sare
Lakini kibaya zaidi timu zote mbili zitataka kushinda mchezo huo kwani mechi zinazofuata wikiendi ijayo zitakuwa ugenini Yanga itakuwa kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ilhali Simba itasafiri hadi Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine kuifuata Tanzania Prisons.
Vipigo vikubwa zaidi ilivyoipata Yanga kutoka kwa Simba bado vipo kwenye kumbu kumbu za mashabiki wa timu hiyo na wamekuwa na matumaini makubwa kuwa ari iliyonayotimu yao inaweza kupoza machungu kwa kurudisha vipigo hivi vya Mei 6 2012 Simba kushinda 5-0 na kile cha Desemba 21 2013 mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo Yanga ilifungwa 3-1 na Simba.
Presha imekuwa kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili hususani wale wa Simba ambao wanakosa furaha kutokana na mwenendo wa timu yao katika mechi tatu zilizopita na ukilinganisha ubora wa wapinzani wao Yanga ambao wameonekana kujipanga kulipiza kipigo cha mabao matano na yale matatu katika mechi ya mtani jembe.
Simba ilikwenda Afrika Kusini Kujiandaa na pambano hilo na wapinzani wao Yanga walibaki Dar es Salaam wakipiga kambi kwenye Hoteli ya LandMark kujiandaa na mechi hiyo kila upande umedhamiria kushinda bila kujali Simba wamesema watazinduka katika mechi hiyo huku Yanga nao wakitamba kuvunja mwiko kwa kulipa kisasi cha mabao 5-0.
Mwamuzi Israel Nkongo ndiye aliyepewa jukumu la kupuliza kipyenga katika pambano hilo lakini mwamuzi huyo amekuwa na bahati mbaya na Yanga kwani alishawahi kupigwa na mchezaji Stevano Mwasika msimu wa 2011.2012,wakati alipokuwa anaichezesha timu hiyo dhidi ya Azam FC iliyoshinda mabao 3-1.
Nkongo mwamuzi mwenye beji ya FIFA,Shirikisho la soka limekuwa na imani kubwa na mwamuzi huyo kwamba ataliendesha na kulimaliza salama pambano hilo na kila upande kuridhika na maamuzi atakayoyatoa kwa dakika zote 90

By Zuberi Karim Jumaa
Shukrani:goal.com

0 comments: