Historia inaonyesha mara nyingi timu hizi zinapokutana ile timu iliyokuwa kwenye kiwango kizuri na inayopewa nafasi ya kushinda ndiyo inapoteza mchezo dhidi ya ile dhaifu
PAMBANO kali kati ya timu zenye upinzani wa jadi Yanga na Simba litafanyika Jumamosi kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa raundi ya nne kwa timu zote mbili zinazishiriki Ligi Kuu Tanzania bara.
Timu hizo zinakutana zikiwa katika hali mbili tofauti Yanga watakao kuwa wenyeji kwenye mchezo huo wa Jumamosi wataingia uwanjani wakuwa hawana presha kubwa kama ilivyo kwa mahasimu wao Simba ambao hawajapata ushindi katika mechi tatu walizocheza msimu huu
Yanga wanakosa presha baaada ya kuwa na ponti sita kufuatia kushinda mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar kule kwenye uwanja wa Jamuhuri Morogoro siku ya ufunguzi Septemba 20.
Mbali na pointi hizo sita lakini kingine kinachopunguza presha kwa Yanga ni uimara wa kikosi walichokuwa nacho na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wao katika mechi nne walizo cheza hivi karibuni ukijumuisha na ile ya Ngao ya Jamii ambayo waliifunga Azam mabingwa watetezi mabao 3-0 kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Niukweli usiyofichika kadiri siku zinavyo karibia za mpambano huo ndivyo mapigo ya moyo pamoja na presha ndivyo vinavyo zidi kuongeza joto kwenye miili ya viongozi na mashabiki wa Simba ambao hawana imani kabisa na kikosi chao pamoja na kwenda Afrika Kusini kupiga kambi kujiandaa na pambano hilo.
Tumaini pekee kwa mashabiki wa Simba katika mchezo huo ni mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi,ambaye amekuwa na jitihada kubwa tangu alirejea kwenye timu hiyo msimu huu akitokea Yanga usajili ambao ulileta utata na kumfanya mchezaji huyo kukosa furaha kutokana na zomea zomea anayokutana nayo kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

Okwi anaonekana kuwa ndiyo tumaini na tegemeo kwa mchezo huo kufuatia kiwango bora alichonacho kwa sasa huku mashabiki hao wakikosa kabisa huduma ya Raphael Kiongera,aliyesajiliwa kwa mbwebwe akitokea KCB ya Kenya baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.
Ukiachana na Okwi katika mchezo huo Simba itategemea zaidi huduma ya wachezaji Shabani Kisiga, Jonas Mkude,Haruna Chanongo,Amri Kiemba Ivo Mapunda ambaye anaripotiwa kuwa fiti baada ya kuvunjika kidole akiwa mazoezini huko Zanzibar na kwenye ushambuliaji itakuwa na Amisi Tambwe ambaye tangu kuanza kwa msimu huu amefunga bao moja tu Septemba 21 dhidi ya Coastal Union.
Pamoja na wachezaji hao lakini bado Simba huwezi kuwalinganisha na wapinzani wao Yanga ambao wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na machaguo ya kutosha kwa wachezaji na pengine kocha Marcio Maximo,akatumia mbinu ile aliyoitumia kuiua Azam kwa kuweka nje silaha nyingine akisubiria kipindi cha pili.

Katika mechi za hivi karibuni Msuva amekuwa katika kiwango cha juu sambamba na Ngasa kasi ya mawinga hawana inaonyesha wazi nama ambavyo mabeki wa Simba watakavyokuwa na kazi ya kuweza kuwadhibiti wachezaji hawa ili wasiweze kupenyeza mipira kwa washambuliaji Geilson Santana Santos JAJA na mwenzake Hamisi Kiiza ama Andrey Coutinho Mbrazili mwingine ambaye amekuwa kwenye uwezo wa juu.
Msimu uliopita timu hizi hazikuweza kufungana kwenye mechi zote mbili za Ligi Kuu baada mchezo wa awali kutoka sare ya 3-3 kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam kisha zikagawana tena poimti kwa kutoka sare ya 1-1,kwenye pambano la marudiano kwenye uwanja ea taifa Dar es Salaam.
Historia inaonyesha mara nyingi timu hizi zinapokutana ile timu iliyokuwa kwenye kiwango kizuri na inayopewa nafasi ya kushinda ndiyo inapoteza mchezo dhidi ya ile dhaifu pengine hiki kinaweza kuwa na nafasi yake kwa sababu mbalimbali kwa huwa kujiamini kunapitiliza zaidi na kujikuta mambo yanakuwa magumu kwao.
Msimu uliopita katika mechi zote tatu walizo cheza ikiwemo ile ya Nani Mtani Jembe Yanga ilikuwa imara zaidi ya Simba lakini mambo yahakuwa kama vile walivyotarajia mashabiki wa timu hiyo baada ya kujikuta wakiambilia sare mbili na mechi moja wakafungwa na Simba ambayo haikuwa ikipewa nafasi kutokana na mapungufu iliyokuwa nayo.
Mechi ya kwanza ya ligi ililazimishwa sare ya 3-3 huku yeyenye ikitangulia kufunga mabao hayo kipindi cha kwanza na kipindi cha pili kiliwabadilikia na kujikuta mabao yote yakisawazishwa na kumaliza dakika 90 matokeo yakiwa 3-3.
Mechi ngingine ilikuwa ile ya Mtani Jembe ambapo Yanga ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kikosi imara ilichokuwa nacho lakini mambo yaligeuka uwanjani na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku bao la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi aliyekuwa anaichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo baada ya kujiunga nayo.

Kwa rekodi hiyo hata pambano la Jumamosi chochote kinaweza kutokea na licha ya uimara unaoonekana kwenye kikosi cha Yanga lakini Simba iliyoanza vibaya kwa kutoka sare na timu tatu dhaifu kwenye ligi ya msimu huu ikashinda mchezo huo na kufufua matumaini ya ubingwa na kuendelea kuionea Yanga katika miaka ya hivi karibuni

Zuberi Karim Jumaa

Thanks:goal.com