MGOMO MKUBWA: Chama cha walimu kuitisha mgomo wa walimu usio na kikomo
Chama
cha walimu wilaya ya MISENYI mkoani Kagera wanatarajia kuitisha mgomo
usiokuwa na kikomo kwa kutofundisha katika shule za msingi na sekondari
endapo uongozi wa halmashauri ya wilaya ya misenyi wataendelea kupoteza
nyaraka zao mbalimbali zikiwemo
Za madai ya malipo na zile za kupandishwa madaraja.
Kwa
mujibu wa taarifa lilyorushwa na ITV ni kwamba baada ya uchaguzi wa
viongozi wa chama cha walimu wilaya ya misenyi wamesema kuwa katika
kikao cha utekelezaji CWT imeutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya
misenyi kutatua migogoro ya waimu katika kipindi cha wiki mbili na
watakapokaidi chama cha walimu kitaitishwa mgomo kwa walimu wote wa
shule za msingi na sekondari bila kujali kuwa wakati huu ni wakati wa
kuandaa wanafunzi kufanya mitihani ya taifa.
Akijibu
malalamiko hayo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi
Bw. Moses Gwaza amekanusha vikali tuhuma hizo na kusema kuwa katika
kipindi cha miezi mitatu serikali imelipa madeni ya walimu katika wilaya
ya Misenyi zaidi ya shilingi miioni 338 na kwamba walimu 96 madai yao
hayapo kwenye bajeti ya mwaka huu na kuwataka kuwa na subira wakati
serikali ikijipanga kuwalipa.
Halimashauri
kuu ya CCM wilaya ya ikungi imemuagiza mkuu wa wilaya hiyo kufuatilia
matumizi mabaya ya shilingi zaidi ya milioni mianne za mfuko wa jimbo la
singida mashariki,jambo ambalo limesababisha miradi mingi ya maendeleo
kushindwa kukamilika.
Akitoa
maadhimio hayo katibu wa CCM wilaya ya ikungi Bwana. Aluu Segamba
amesema baada ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya zote
walibaini jimbo la singida mashariki lina matumizi mabaya ya mfuko wa
jimbo ,huku fedha hizo ni za serekali na zinatakiwa kuwanufaisha
wananchi wote bila kujali vyama vya siasa.
Katika
hatua nyingine Bwana. Segamba amewaomba baadhi ya viongozi wa dini
wenye tabia ya kuingilia maswala ya siasa waache kuongoza dini zao na
waingie kwenye ulingo wa siasa,pia ameiomba serekali wilayani ikungi
kukaa na viongozi hao iliwakawaeleze waumini wao kujitokeza
kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura na kuacha
kuwashawishi waumini kupigia kura katiba ndiyo au hapana,kwa kufanya
hivyo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
kwa
upande wake mkuu mpya wa wilaya ya ikungi,Gishuli Charles,ameahidi
kuzifanyia kazi tuhuma hizo zilizotolewa na CCM,ili kujijengea mazingira
mazuri ya kuchukua hatua za kisheria endapo atajiridhisha na tuhuma
hizo.
thanks:eddy blog
0 comments: