Saudia yakataa tumbili wa Sweden Kisa ?
Saudi Arabia imekatalia mbali tumbili wanne kutoka Sweden kufuatia tofauti za kidiplomasia.
Tumbili
hao wanne ambao ni kutoka jamii ya Amazonia ya tumbili wadogo zaidi
duniani walikuwa msaada kutoka hifadhi ya wanyama ya Skansen iliyoko
Stockholm.Afisa mkuu wa hifadhi hiyo Jonas Wahlstrom anasema kuwa tumbili hao walikuwa wanapaswa kupelekwa katika hifadhi ya wanyama ya Riyadh .
"hawataki tumbili hao tena kufuatia utata uliopo wa kisiasa'' alisema Wahlstrom.
Mwezi uliopita Saudi Arabia ilimuondoa balozi wake huko Sweden baada ya taifa hilo la bara Uropa kukatiza mkataba wa uuzaji wa silaha kwa himaya hiyo.
Tumbili hao wanauzani mdogo sana wa takriban gramu 100 pekee.
Mwezi uliopita Saudi Arabia ilimzomea waziri wa maswala ya kigeni wa Sweden Margot Wallstrom kwa kuingilia maswala ya ndani ya Saudia.
Saudi Arabia ilikasirishwa sana na matamshi ya balozi huyo hadi ikapiga turufu na kumzuia kuzungumza katika jumuia ya Waarab huko Cairo.
chanzo:bbcswahili
0 comments: