UTATA MPYA PAMBANO LA MAYWEATHER, PACQUIAO, KUMBE MYWEATHER ALIPEWA USHINDI KIMAKOSA ~ MBONDE MEDIA

...................






Karatasi
ya matokeo ya majaji watatu Glenn Feldman, Burt Clements na Dave
Moretti zinavyoonyesha na picha inawaonyesha mabondia hao katika kona
zao, Floyd Mayweather ya bluu (kushoto) na Manny Pacquiao nyekundu
(kulia).



Floyd Mayweather akiwa amekaa kona nyenye rangi blue.
Pacquiao akiwa amekaa kona yenye rangi nyekundu.
UTATA umeibuka kutoka Pambano la Karne baina ya
Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika juzi ukumbi wa MGM
Grand, Las Vegas, Marekani.



Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu,
Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia
aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati
mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu,
Mayweather ndiye mshindi.



Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo
na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa
Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu?



Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi
kimakosa bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man
aliyekuwa anatokea kona nyekundu.




UTATA MPYA PAMBANO LA MAYWEATHER, PACQUIAO, KUMBE MYWEATHER ALIPEWA USHINDI KIMAKOSA ~ MBONDE MEDIA http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: