HII NDIO IDADI KAMILI YA WANACHAMA WA CCM WALIORUDISHA KADI ZA UANACHAMA NA KUHAMIA CHADEMA

...................


Muda huu ninapoandika haya madiwani wote wa jimbo la Monduli waliokuwa wa CCM wamerudisha kadi na kujiunga na CHADEMA...
Sio hao tu bali hata wenyeviti wa vijiji na vitongoji wote wa CCM wamerudisha kadi na kujiunga chadema

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


MAAMUZI MAGUMU YA KUTOKA CCM LEO NI MAADILI YALIYOTUKUKA.

Sio uamuzi mwepesi ila ni uamuzi makini na wa Busara tunaofanya leo tarehe 18 Julai 2015. Tumewaiteni hapa leo nyie Waandishi wa habari ili kuutangazia Umma kuwa tumeamua kuondoka na kujivua Uwanachama wa chama cha mapinduzi (ccm) na kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )

Tumetafakari usalama wetu ndani ya ccm kwa umoja wetu kama tulivyo hapa leo lakini tumeshindwa kuuona , ccm iliyokuwa inaongozwa na Katiba, Kanuni na Miongozo mbali mbali ya chama , sasa inaongozwa kwa matakwa ya familia chache kwa jinsi watakavyoona wao inawapendeza.

Ni wazi kabisa kuwa ccm imekosa maadili hivyo inapaswa kufunzwa maadili, kujivua uanachama ni mojawapo ya njia muhimu ya kuifunza ccmnidhamu , tunafahamu kuwa kila Mtu anatambua uchakachuaji wa Kanuni , Katiba na Mwongozo wa Maadili ulivyo hujumiwa katika mchakato wa kumpata Mgombea Urais ndani ya ccm.

Tumeishi kwa muda mrefu ndani ya ccm tukiwa wavumilivu wa matendo ya hila ya baadhi ya Viongozi wa ccm, lakini tuliamini kuwa iko siku pengine tutarekebisha mfumo ndani ya Chama na siku moja kuwa na Serikali mathubuti , kwa hali ilivyo sasa ndani ya ccm jambo hili haliwezekani , ccmimeamua kuua ndoto , mipango na fikra zote za Wanachama wake wanaotafakari Uongozi ndani ya Chama na Serikali katika siku za usoni .Chama kinatuzuia kufikiria malengo yetu na ndoto zetu kwa kuamua kupuuza utaratibu wa Kikatiba na Kisheria , na sisi tunakosa Amani na hivyo hatuwezi kamwe kama Binadamu wenye mawazo chanya kuishi ndani ya mfumo wa namna hii.Wanachama wa ccm hawana uwezo wa kupanga mipango na kufikiria siku zao za baadaye katika Siasa wala hawana mamlaka tena ya kumchagua Kiongozi wanayemtaka , yaliyomkuta mmoja wa Wagombea Mh Edward Lowasa na wenzake ni ishara kuwa Mwanachama yeyote wa ccm kuanzia sasa hawezi kuwaza wala kufikiri malengo mapana ndani ya Chama. Kwani Uamuzi ndani ya ccm hauzingatii tena Utaratibu na vikao vya Kikatiba bali maelekekezo na utashi wa familia chache.

Hivyo basi tunakataa kuwa Watumwa katika misingi hii na ndio maana leo tunaondoka sisi Viongozi wote tulioko hapa pamoja na Wananchi wengi tunao wawakilisha. Tumeamua kujiunga rasmi na CHADEMA , tunafahamu kuna hofu kubwa tunayojaribu kupandikiziwa , lakini hata hivyo tumejipanga kukabiliana na kila uovu katika hatua yetu hii ya Kidemokrasia, hakuna tunaye muogopa , hakuna anayetutisha na hakuna hatakayeweza kutuzuia kwenye Safari yetu hii inayoendelea . Tuna uhakika wa kushinda tena Uchaguzi wa Kata zote’ pamoja na Jimbo la Monduli na Nchi kwa ujumla kwa Chama chetu CHADEMA. 

Tunamuomba Mh Lowasa aungane nasi katika Safari yetu hii inayoendelea, awe na Moyo wa Ujasiri wa kufanya maamuzi magumu, hakuna busara nyingine anayoweza kutumia zaidi ya kuondoka ccm . Na huu ndio utakuwa uamuzi makini, mgumu kama ambavyo amekuwa akisema mara nyingi, aidha huu utakuwa uamuzi wenye tija sana kwake, kwa Jimbo la Monduli na kwa nchi yetu.

Ushauri wowote wa kuilinda ccm anaopewa ni ushauri batili , Watu wote wanaomfuata sasa walipaswa kuishauri ccm huko nyuma walipoona uvunjwaji wa Katiba , Taratibu , Maadili na Kanuni unafanyika , lakini badala yake walishangilia na kufurahia kwa niaba ya Familia chache.Tutaiangusha ccm , kama Kenya walivyoiangusha KANU ,wakati ni sasa . Sasa tunaanza ziara ya kuingusha ccm , tumedhamiria , tunahitaji na tunaweza . 

Tunawataka wafuasi wetu wote mahali popote walipo pindi watakaposikia tamko hili wachukue maamuzi mara moja ya kuachana na ccm na kujiunga rasmi na CHADEMA na kuendelea kusambaza ujumbe huu.

Tunamkaribisha Mh Lowasa CHADEMA kwa kumkumbusha maneno aliyosema Hayati Nelson Mandela “ I learned that courage was not the absence of fear, but the triumph over it. The brave man is not he who does not feel afraid, but he who conquers that fearAsanteni sana kwa kutusikiliza “ Maadili yaliyokosa maadili yanapaswa kufunzwa Maadili”
Nimesoma tamko hili leo tarehe 18 Julai 2015 kwa niaba ya wenzangu wote tuliosaini katika kiambatanisho kwenye taarifa hii
Bado kuna mbunge ambaye inasemekana kajiuzuru chama hicho tutakapo pata uhakika tutawajulisha


chanzo:specialsweetnesstz255.blogspot.ca
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: