YAWEZEKANA YUDA KUWA YESU...?

...................
Jambo linalofanywa sasa ni kudhihirisha siasa ni mchezo mchafu. Lowassa awa dili kwa chadema japo walimwita fisadi mwizi na sifa nyingine mbaya

Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.


Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu 

CHANZO:www.thechoice.us
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: