MAALIM ATOA KAULI NZITO JUU YA LIPUMBA : SOMA HAPA.....!
Wafuasi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na pia mwenyekiti mwenza wa muungano wa wapinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba, wameanza kushughulikiwa na kutakiwa kuchagua moja; kuendelea kuwa ndani ya chama hicho au kutoka.
Ingawa
Profesa Lipumba alipojiuzulu uenyekiti, alisema ataendelea kuwa
mwanachama wa CUF, lakini Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif
Hamad amewataka wanachama waliokuwa wakimuunga mkono, kuamua moja,
kubaki ndani ya chama hicho kama alivyoamua mchumi huyo mashuhuri
duniani, au kutoka.
“Profesa Lipumba kajiuzulu CUF, wale waliojiunga CUF kwa sababu ya Profesa, wanayo fursa ya kuamua kubaki CUF au kutoka,” alisema Hamad juzi usiku.
Mbali
na kuwataka wanaomuunga mkono Profesa Lipumba kuamua kutoka ndani ya
chama hicho au kubaki, wakati kiongozi wao akiwa ameweka wazi kuwa hana
nia ya kutoka katika chama hicho, Maalim Seif alitoa kauli zingine
kuashiria kutohitaji hata uanachama wa Lipumba ndani ya CUF.
“Kama
ni treni inayokwenda Mwanza, ikifika Morogoro abiria watashuka, lakini
wengine watapanda, ikifika Kaliua watashuka abiria lakini wengine
watapanda,” alisema Maalim Seif alipofanya ziara ya ghafla katika Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam juzi usiku.
Hamad
amewahakikishia wanachama wa chama hicho waliokuwa wamezingira ofisi
hiyo, kuwa uamuzi wa Profesa Lipumba kujiuzulu wadhifa wake
hautausambaratisha Ukawa na CUF, ambayo kwa sasa haina Mwenyekiti wala
Makamu Mwenyekiti, lakini akasema imeendelea kubaki katika mikono
salama.
Alisema
akiwa Katibu Mkuu na viongozi wenzake waliobaki, watahakikisha kwamba
chama hicho kinafikia malengo ya kuanzishwa kwake, ambayo ni kuhakikisha
kinakamata dola.
Alisema
mwishoni mwa wiki hii, chama hicho kitaanza vikao vyake kuzingatia
hatua iliyotokea, ili wachukue uamuzi thabiti wa kukiongoza chama hicho
na kuhakikisha kinabaki katika mikono salama, hadi hapo uchaguzi wa
kumtafuta Mwenyekiti utakapofanyika.
Akizungumzia
Ukawa, Hamad alisema baada ya hatua hiyo ya Profesa Lipumba,
alizungumza na viongozi wakuu wa umoja huo, akiwemo Freeman Mbowe
(Mwenyekiti wa Chadema), James Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na
Emmanuel Makaidi (Mwenyekiti wa NLD) pamoja na mgombea urais wa umoja
huo, Edward Lowassa na wamehakikishiana kuwa hawatarudi nyuma.
“Tumehakikishiana
kwamba Ukawa upo na umeimarika zaidi na hatutarudi nyuma… Tumeona kwa
namna unavyoungwa mkono na wananchi walio wengi, Magufuli (mgombea urais
wa CCM) Ikulu ya Magogoni hataiona,” alidai Maalim Seif.
chanzo:kibonajoro
0 comments: