Utajiri wa Aliko Dangote washuka kwa zaidi ya asilimi 35

...................

Alio Dangote, Rais na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Dangote Group, nchini Nigeria.Creative Commons
Utajiri wa tajiri mkubwa zaidi barani Afrika raia wa Nigeria Aliko Dangote, umeshuka kwa asilimia 35 hadi kufikia kiwango cha dola za Marekani bilioni 9.9, kutokana na kushuka kwa thamani ya Naira na kuporomoka kwa bei ya madini katika soko la dunia, taasisi ya Bloomberg imesema.
Dangote ni miongoni mwa watu wenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika, ambapo kwa takwimu za hivi karibuni anashikilia nafasi ya kwanza barani Afrika, akifuatiwa na raia wa Afrika Kusini, Christo Wiyese, ambaye utajiri wake umekuwa kwa asilimia 12 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Aliko Dangote amewekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa viwanda vya Simenti, Sukari, Unga, Viwanda wa nguo, Kilimo na hivi karibuni kwenye sekta ya kibenki.
Mwezi Agosti mwaka huu, Dangote amezindua rasmi benki yake ya kwanza ambayo inaendeshwa kidijitali nchini Nigeria, ambapo watu takribani milioni 40 waliokuwa wanatumia mfumo wa kawaida wa kibenki wameanza kuhamia kwenye benki yake.
Benki hiyo ambayo imepewa jina la SunTrust, imeshapewa leseni ya uendeshaji wa kimataifa kutoka kwa benki kuu ya Nigeria, huku makao yake makuu yakiwa jijini Lagos.
Benki hiyo tayari imeanza kutoa huduma zake kwa njia ya kielektroniki kama vile kutumia simu ya kiganjani au mtandao Internet.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa beni hiyo, Dangote amesisitiza kuwa, njia hizi za kielektroniki zitaifanya SunTrust kuwa benki yenye makusanyo makubwa kutokana na huduma zake za bei nafuu tofauti na benki nyingine nchini humo, amenukuliwa na taasisi ya Ecofin.
Kuanzishwa kwa aina hii ya benki, kunatokana na ukweli kwamba mfumo wa kawaida ni mzito hasa kwa vile unatumia utaratibu wa kuwa na matawi ambao ni unagharama kubwa na mapato yake ni finyu.


Mfanyabiashara huyo akaongeza kuwa, mfumo huu utawafanya wateja wake kufanya miamala ya fedha wakiwa majumbani mwao na hivyo kuokoa muda na gharama zisizo za lazima.
Dangote amepoteza kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.7 katika siku moja ya Jumatatu ya Juni 20 mwaka huu, kufuatia kuporomoka kulikopindukia kwa Naira kulikosababishwa na mzozo wa kisiasa, kushuka kwa uzalishaji wa mafuta, kushambuliwa kwa miundombinu ya mafuta pamoja na kushuka kwa thamani ya Naira dhidi ya dola ya Marekani.
Tangu kushuka kwa thamani ya Naira, orodha mpya ya matajiri duniani iliyotolewa hivi karibuni, imeonesha Dangote ameshuka kwa nafasi 25 kutoka nafasi ya 46 hadi kufikia nafasi ya 71.
Jumla ya utajiri wake sasa, ambao unakadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 12.7 unatokana kwa asilimia 91 na ushiriki wake katika kampuni ya “Dangote Cement”.
Kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kunaifanya nchi ya Nigeria, kupungukiwa pato la ndani, sekta ambayo ilikuwa inategemewa kwa zaidi ya asilimia 90, na hali hii imekuwa ni pigo kubwa kwa uchumi wa Nigeria tangu mdororo wa kiuchumi ulioshuhudiwa kwenye miaka ya 90.
Ili kuirejeshea Naira uimara wake, mwaka uliopita Serikali iliamua kuifanya thamani ya Naira kubaki kwa kiwango kisichobadilika sawa na dola moja ya Marekani kwa vile Rais Muhamadu Buhari, aliamini kuwa kuanguka kwa thamani ya Naira kungeua uchumi wa taifa hilo.

 chanzo:http://sw.rfi.fr
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: