RAIS KIKWETE AWAITA AZAM FC IKULU NA KUWAAMBIA; “LETENI KOMBE LA AFRIKA HAPA”

...................


Rais Kikwete akiwa na wachezaji na viongozi wa Azam FC leo Ikulu mjini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amewataka wachezaji wa timu ya Azam kuhakikisha mwakani wanachukua ubingwa wa Afrika na si kuridhika na kikombe cha Kombe la Kagame ambalo walishinda Jumapili iliyopita hapa jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliwaambia wachezaji hao leo jioni walipokwenda Ikulu kumkabidhi kikombe hicho walichoshinda baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali.
Akizungumza na wachezaji hao, Rais Kikwete amewataka kutoridhika na ubingwa huo wa Kombe la Kagame na sasa maandalizi yao yawe ni kujipanga kushinda ubingwa wa Afrika na si kutolewa kwenye hatua za awali za mashindano hayo.
Aliwaambia kuwa ushindi wao umewapa furaha Watanzania wengine na kuwafuta 'mchanga wa macho' mashabiki wa soka hapa nchini ambao wanaupenda mchezo huo.
Aliwataka waendelee kujiimarisha zaidi na kutokuwa na klabu nyingin ambazo viongozi wake huendesha timu kama vile Simba na Yanga zinavyojiendesha.
Alisema baada ya kusikia Azam imeshinda alifurahi na kuongeza kwamba ushindi huo umepunguza ukame wa vikombe vya mashindano ya kimataifa kwa klabu za hapa nchini.
"Hongereni sana, maana mmeshinda, ingekuwa wengine wangeanza kutoa sababu ambazo si za kimpira, mara marefa, mchezaji mmoja kupakaziwa, angalau mmepunguza ukame wa vikombe", alisema.
Aliwataka Azam kuhakikisha mwakani wanashinda tena kikombe hicho hadi kufikia mara tatu na hatimaye kuwa chao moja kwa moja.
Rais Kikwete akiwa na Azam FC Ikulu Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Azam, Said Mohammed, alisema kuwa ushindi wa timu yao umetokana na nasaha ambazo Rais Kikwete aliwapa wakati wa uzinduzi wa kituo chao cha Azam Complex.
Mohammed alisema kuwa wanamuahidi wataendelea na juhudi zao katika msimu ujao wa ligi na mashindano mengine watakayoshiriki.
"Lengo letu ni kushinda kikombe cha Afrika", alisema mwenyekiti huyo.
Alimweleza pia Rais Kikwete kwamba Azam imeweka rekodi ya kushinda kikombe ikiwa ni timu ambayo haijafungwa bao hata moja wala kupoteza mchezo.
 
chanzo:bin zubery blog
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: