CCM YAPATA PIGO,MGOMBEA WAKE WA UDIWANI AFARIKI DUNIA GHAFLA.
Chama
cha Mapinduzi Jimbo la Mbeya Mjini kimepata pigo baada ya mgombea wake
wa Kata ya Uyole, Kambi Njela , pichani juu) kufariki dunia ghafla.
Njela
ambaye alianza kampeni mwezi uliopita aliugua ghafla akiwa anaendelea
na kampeni zake na kwamba dalili za ugonjwa zilianza kwenye miguu ambayo
ilionekana kupata ubaridi na hatimaye homa kali.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Mbeya, Ephrahimu Mwaitenda amesema kifo hicho ni pigo
kubwa kwa chama hicho kwani marehemu alipita bila kupingwa kwenye kura
za maoni, hivyo tayari walikuwa na ushindi mkononi
Naye
meneja wa Kampeni za CCM Wilaya ya Mbeya mjini,Charles Mwakipesile
amesema kuwa marehemu alikuwa mchapa kazi na aliweza kuisimamia vizuri
Ilani ya chama chake katika kata yake na ndiyo ilikuwa inaongoza kwa
maendeleo.
“Alifanya
vizuri kwenye kata yake na ndiyo maana hakuweza kupata upinzani na
hatimaye kupita bila kupingwa hivyo tumempoteza mtu muhimu sana ndani ya
chama na tumeipoteza kata hiyo ambayo tayari ilikuwa mikononi
mwetu”amesema Mwakipesile
Kwa
upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbeya, Musa Zunguza amesema
kutokana na kifo hicho taratibu zinafanyika kusimamisha kampeni za
udiwani kwenye kata hiyo
chanzo:magicnewstz.blogspot.com
0 comments: