Mtoto adhaniwa kupeleka bomu shuleni
Raisi Barrack Obama
amemualika ikulu mvulana wa kiislamu mwenye umri wa miaka 14 mara baada
ya kushikiliwa na polisi kwa muda baada ya kupeleka shuleni saa
aliyoitengeneza mwenyewe nyumbani na mwalimu wake kudhania kuwa ni bomu.
Kupitia
ukurasa wa twitter Raisi Obama alimsifu Ahmed Mohamed kwa saa yake hiyo
na kuwataka watoto wengine kuhamasika na kufurahia sayansi kama Ahmed.
Hapo
jumatatu kijana huyo alishikiliwa na polisi baada ya mwalimu wake
alipotoa taarifa polisi kuhusu chombo alichokuja nacho shuleni.
kikundi cha kiislamu nchini Marekani kilizungumzia suala hilo kuwa kijana huyo alikamatwa kwa kuwa ana Imani ya Kiislamu.
Taarifa ya kukamatwa kwake kulileta hisia tofauti katika mitandao ya kijamii
chanzo:bbcswahili
0 comments: