Man Utd kucheza mechi kwa heshima ya Rooney

...................


Klabu ya Manchester United imekubali kucheza mechi maalum kwa heshima ya nyota wake Wayne Rooney, ambaye ameahidi mapato kutoka kwa mechi hiyo yatatumiwa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
Klabu imekubali kucheza mechi hiyo baada ya mashabiki kuiandikia barua ikitaka mchango wa Rooney utambuliwe kwa njia maalum.
Mechiyo itachezewa Old Trafford Agosti 2016, dhidi ya wapinzani ambao watateuliwa baadaye.
"Siku ya mechi hiyo itakuwa muhimu sana kwangu na kwa familia na natumai nitaweza kushangaza watu kwa jambo moja au mawili," amesema Rooney.
Naibu mwenyekiti wa United Ed Woodward amesema: "Kuanzia mabao yake matatu aliyofunga mechi yake ya kwanza hadi hadi bao la majuzi zaidi la kufikisha mabao 236, Wayne amekuwa nguzo kuu katika kipindi chenye ufanisi sana historia ya klabu hii.”
Mapato kutoka kwa mechi hiyo yatakabidhiwa vituo mbalimbali vya kusaidia watoto, kupitia wakfu wa Wayne Rooney.
Habari hizo zimetolewa huku Rooney, aliyesherehekea siku yake ya 30 ya kuzaliwa Oktoba 24, akikosolewa sana kutokana na uchezaji wake hivi karibuni.
Baada ya kutoka sare tasa na Manchester City Jumapili, meneja wa United Louis van Gaal alisema amechoshwa na kuulizwa maswali kuhusu mchezaji huyo, ambaye ndiye aliyemteua nahodha msimu wa 2014-15.
Rooney amefunga mabao mawili Ligi ya Premia mechi tisa msimu huu, ingawa alifunga matatu mechi ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya FC Bruges mwezi Agosti.
Amefunga jumla ya mabao 236 tangu awasili Old Trafford akitokea Everton kwa £27 mwaka 2004. Amepitwa tu na Sir Bobby Charlton (249) na Denis Law (237) katika kufungia klabu hiyo mabao mengi zaidi

CHANZO:BBCSWAHILI

http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: