kwa habari zaidi ingia link hii http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151023_uchaguzi2015-tanzania-yaamua
8.36am:Takriban wapiga kura milioni 22,750,789 wanashiriki katika shughuli hiyo.
7.50am:Huku shughuli ya upigaji
kura ikiendelea maeneo mengi yamesalia kuwa mahame zikiwemo barabara na
maeneo mengi ya mji wa Dar es Salaam.Hii ni kwa sababu raia wengi
wanashiriki katika shughuli hiyo.
7.14am:Katika kituo cha Dodoma
foleni ndefu imeshuhudiwa ,ni kituo kilichopo katikati ya mji.Baadhi ya
wapiga kura waliofika kituoni humo na kupiga kura wanasema hakuna tatizo
lolote walilopata.
7.13am:Katika kituo cha
kinondondoni tayari watu wameanza kupiga kura bila matatizo
yoyote.Sheria ya mita 200 inaonekana kuanza kuheshimiwa kwani watu
wanapiga kura na kuondoka vituoni
7.05am:Mtafarufuku
umetokeo katika kituo cha masaki baada ya maafisa wa uchaguzi kutoka
nje ya vituo vya kupiga kura na kuwaelezea raia kupanga mistari mitatu
inayowapendelea wanawake,na wazee.Wengi wa wale waliofika mapema
wamepinga hatua hiyo wakidai kwamba ni haki yao kupiga kura wa kwanza.
7.00am:Ni saa moja kamili saa za Afrika mashariki na wakati muhimu kwa taifa la Tanzania ambapo shughuli ya upigaji kura inaanza rasmi 6.30am:Waangalizi wa kimataifa
tayari wamefika katika vituo vya kupigia kura katika maeneo mbalimbali
nchini Tanzania ili kushuhudia matukio ya uchaguzi huo.
6.30am: Ili kutaka kufahamu iwapo jina lako liko katika sajili ya uchaguzi wengi wamekuwa wakipiga nambari hizi *152*00# 6.15am:Usalama umeimarishwa katika kila kituo kulingana na maripota wetu wanaofuatilia matukio mabli mbali ya uchaguzi huu.
6.10am:Maripota wetu wamesambazwa kila maeneo ya taifa hilo ili kuweza kukupatia habari za moja kwa zinazojiri katika maeneo hayo.
6.0am:Wengi wa watu wamewasili
katika vituo hivyo mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ili kupata fursa
ya kupiga kura hiyo mapema na kuelekea majumbani mwao ili kufuatilia
uchaguzi huo katika vyombo vya habari.
6.03am:Tayari maelfu ya watu
wamejitokeza katika vituo mbali mbali vya kupigia kura nchini humo ili
kushiriki katika zoezi hilo linalotarajiwa kuanza saa moja asubuhi.
6.01am:Ni
asubuhi njema na siku muhimu kwa raia wa taifa la Tanzania ambapo raia
wanapiga kura kumchagua atakayemrithi rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho
Kikwete
6.00am:Habari ya asubuhi.
TANZANIA YAAMUA.
19:18pm: Waangalizi wa uchaguzi kutoka eneo la
Maziwa Makuu wamesema wamefurahishwa na maandalizi ya uchaguzi.
19:11pm: Zikiwa
zimesalia saa machache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania
kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo imesema kuwa maandalizi
ya shughuli hiyo yamekamilika.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151023_wagombea_urais_wote_tanzania
18:00pm: Muda rasmi wa kufanya kampeni umemalizika na sasa kazi ni kusubiri saa moja Oktoba 25 kura zianze kupigwa.
Watanzania
wanapiga kura Oktoba 25 kumchagua mrithi wa Rais Jakaya Kikwete
anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
0 comments: