SPEA ZA MASHINE ZA MRI NA CT-SCAN ZIMEFIKA NA MATENGENEZO YAMESHAANZA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari
leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya
kufuatilia agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye awali aliagiza
wagonjwa wasilale chini. Rais Magufili aliitembelea Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili (MNH) hivi karibuni na kutoa agizo hilo. Leo Balozi Sefue
ameitembelea mashine ya MRI, ST-Scan na Jengo la Taasisi ya Mifupa ya
MOI. Akiwa katika ofisi ambako ipo mashine ya MRI na ST-Scan Balozi
Sefue amepewa taarifa ya matengenezo ya mashine hizo.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa
agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na
kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye
vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
Katibu
Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa
mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo
imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica
Joseph ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
Mmoja
wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa
Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine
hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
----
SERIKALI Kuendelea Kuboresha Sekta ya Afya Nchini Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya ziara katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema
serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza
baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema amekagua mashine za MRI
na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza
mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania
imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na
Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando
itapata mashine moja ya MRI.
Pia,
amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima
ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia
kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema
ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama na kuwa na
maduka yao ya ndanichanzo: matukiotz.co.tz
0 comments: