Yaliyojiri Leo Tanzania:Rais John Pombe Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Hazina Kuu

...................


Ikiwa ni siku moja toka aapishwe kushika uongozi wa nchi yetu, rais ameanza kazi ya kututumikia kama alivyotahidi katika kampeni kuwa hata tuangusha.

Rais mpya wa Tanzania John Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Hazina Kuu siku moja tu baada yake kuapishwa.
Rais huyo amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Bw Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka huu baada ya kujiuzulu kwa George Werema.
Bw Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuna uwezekano amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi.
Wakati wa kampeni, Bw Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari.
Bw Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: