Mafisadi 12 waliohusika na wizi wa Makontena Bandarini watajwa...
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Dar es Salaam.
Kufuatia agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar
es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo
limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar
es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani
Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika
makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao
wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi
utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali
ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja
Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu
wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi
Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun
Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi
wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la
Polisi katika kutekeleza majukumu yake.
0 comments: