Dangote na Bill Gates kukabili utapia mlo Nigeria

...................



Image captionDangote na Bill Gates
Mfuko wa hazina ya Bill na Melinda Gates pamoja na ule wa Dangote umeingia katika mkataba wa ushirikiano unaogharimu dola milioni 100 kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa wa utapia mlo nchini Nigeria katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Mkataba huo uliafikiwa mjini Abuja na rais wa kampuni za Dangote,Aliko Dangote ambaye alitia sahihi mkataba huo kwa niaba ya hazina ya Dangote huku Bwana Bill Gate akitia sahihi kwa niaba ya hazina ya Bill na Melinda Gates.
Makubaliano hayo yalishuhudiwa na wanachama wa jamii ya kimataifa pamoja na maafisa wa serikali ya Nigeria.
Akizungumza kabla ya kutiwa sahihi kwa mkataba huo, waziri wa afya nchini humo profesa Issac Adewale ameonya kwamba asilimia 10 ya idadi ya watu milioni 170 wanakabiliwa na utapia mlo, na wengi wao wanaishi katika majimbo yenye vita ya Kaskazini mashariki.
Aliko Dangote kutoka Nigeria ambaye ni mtu tajiri barani Afrika,amesema kuwa changamoto kuu inayowakabili katika harakati za kumaliza vifo miongoni mwa watoto ni utapia mlo.
Kulingana na yeye, taifa hilo lina idadi kubwa ya visa vya utapia mlo duniani vikiwa asilimia 18.
Hatahivyo amesema kuwa hazina zote mbili zina mipango kabambe ya kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba zitafanya kazi kwa ushirikiano ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa lishe bora nchini Nigeria kuanzia sasa hadi mwaka 2020.
Mwanzilishi mwenza wa hazina ya Bill na Melinda gates Bill gates amesema kuwa ijapokuwa si rahisi kukabiliana na tatizo hilo ni muhimu katika siku za usoni.
Amesema kuwa kufuatia majadiliano waliofanya na mamlaka ya Nigeria,ana matumaini kwa kile ambacho mkataba huo utaafikia
chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: