Huenda rais Putin 'aliidhinisha' mauaji ya Jasusi

...................



Image copyrightGetty
Image captionLitvinenko
Mauaji ya aliyekuwa jasusi wa Urusi Alexander Litvinenko mwaka 2006 nchini Uingereza huenda yaliidhinishwa na rais Vladimir Putin ,kulingana na uchunguzi.
Bwana Putin huenda alitia saini sumu ya mauaji ya bwana Litvinenko ya polonium-210 kutokana na uhasama kati yao, ulisema uchunguzi.
Mjane wa Bwana Litvinenko,Marina aliunga mkono ripoti hiyo akitaka bwana Putin kuwekewa marufuku ya usafiri huku Urusi ikiwekewa vikwazo.
Hatahivyo waziri wa maswala ya kigeni wa Urusi amesema kuwa uchunguzi huo umeingiliwa kisiasa.
''tunajuta kwamba kesi hiyo ya uhalifu imeingiliwa kisiasa na kuathiri mazingira ya uhusiano wa kibishara''.
Image copyrightGetty
Image captionBi Litvinenko
Amesema kuwa Uchuguzi huo haukuwa wazi hivyobasi hawakudhania kwamba matokeo yake hayangekuwa na upendeleo.
Bwana Litvinenko alifariki akiwa na umri wa miaka 43 mjini London mwaka 2006,siku kadhaa baada ya kuwekewa sumu.
Alikuwa jasusi wa zamani wa Urusi lakini alitorokea nchini Uingereza ambapo alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Putin.
Mwanadishi wa BBC wa maswala ya usalama Gordon Corera,amesema kuwa kulikuwa na mshangao mkubwa ndani ya mahakama wakati ripoti hiyo ilipotolewa.
Akizungumza nje ya mahakama ya London,bi Litvinenko alisema:Maneno ambayo mume wangu alizungumza katika kitanda chake cha mauti akimshtumu bwana Putin yamethibitishwa na mahakama moja ya Uingereza.
Image copyrightReuters
Image captionBwana Litvinenko 1998
Katika taarifa,bi Litvinenko aliitaka serikali ya Uingereza kuwatimua majasusi wote wa Urusi na kuiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi.
Aliongezea kwamba bado ana matumaini kwamba haki itapatikana kwa wale waliotekeleza kifo hicho.
Katibu wa maswala ya ndani nchini Uingereza Theresa May anatarajiwa kutoa jibu la ripoti hiyo kwa serikali ya Uingereza katika ripoti yake kwa bunge la Uingereza.

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: