KORTINI KWA KUMTUKANA MKE WA RAIS
Mbunge ashtakiwa kumtusi mke wa Mugabe
Mbunge mmoja wa
chama tawala nchini Zimbabwe anatarajiwa kufikishwa kortini kujibu
mashtaka ya kumtusi mke wa Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe.
Mbunge
huyo Bw Justice Wadyajena anadaiwa kutumia “lugha ya matusi” dhidi ya
mwanachama mwenzake wa chama tawala cha Zanu-PF aliyekuwa ameweka picha
ya Bi Mugabe kwenye gari lake.Kisa hicho kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92 Februari.
Bw Wadyajena amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi Muduvuri: "Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa kortini Victoria Falls.
Mke wa rais nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa chama cha Zanu-PF.
Mbunge huyo amekanusha madai hayo.
chanzo:bbcswahili
0 comments: