ATOWEKA KAZINI MIAKA SITA
Mtumishi wa umma nchini Uhispania amepigwa faini baada ya kugunduliwa kwamba hakuwa amefika kazini kwa miaka sita.
Amepigwa faini ya €27,000 (£21,000; $30,000).
Joaquin Garcia aligunduliwa baada yake kuanza kutafutwa apewe tuzo ya kutumikia serikali kwa muda mrefu.
Mfanyakazi
huyo wa umri wa miaka 69, ambaye kazi yake ilikuwa kusimamia
wafanyakazi katika kiwanda cha kushughulikia maji taka mji wa Cadiz,
sasa amestaafu.
Amekanusha tuhuma dhidi yake na kusema 'anazingiziwa na kwamba alikuwa anadhalilishwa.
Bw Garcia alilipwa €37,000 kila mwaka kabla ya kutozwa ushuru.
Kampuni
hiyo ya maji ilidhani alikuwa akisimamiwa na serikali ya mtaa nayo
serikali ya mtaa ilidhani alikuwa akisimamiwa na kampuni hiyo.
Naibu
meya aligundua Bw Garcia alikuwa hafiki kazini baada yake kuanza
kutafutwa apewe zawadi kwa kutumikia serikali ya mtaa kwa miaka 20.
Faini aliyotozwa inatoshana na mshahara wake wa mwaka mmoja baada ya kutozwa ushuru.
Mahakama imekubali mashtaka dhidi yake na kuagiza alipe faini hiyo
chanzo:bbcswahili

0 comments: