FACEBOOK YATUMIKA KUWAPATA WATOTO KWAAJILI YA MAPENZI
Wanaowatamani watoto kingono watumia facebook
Watu wanaowatamani watoto kingono watumia mitandao
Watu wanaowatamani
kingono watoto wadogo wanatumia makundi ya siri katika mtandao wa
facebook kuchapisha na kubadilishana picha chafu za watoto ,BBC
imebaini.
Hali ya ulivyopangwa mtandao huo wa kijamii unayaficha
makundi hayo kwa wateja wengi na ni wanachama pekee ambao wanaweza kuona
yanayoendelea.Kamishna wa watoto nchini Uingereza Anne Longfield amesema kuwa facebook haifanyi juhudi za kutosha kuyazuia makundi hayo ili kuwalinda watoto.
Uchunguzi wa BBC umebaini idadi ya makundi kadhaa ya siri ,yaliobuniwa na kuendeshwa na wanaume wanaowatamani kingono watoto wadogo likiwemo moja ambalo linaendeshwa na mwanamume mmoja aliyefungwa kwa kuwatamani watoto wadogo na ambaye hadi sasa yupo katika orodha ya wahalifu wa ngono.
Makundi hayo yana majina yanayoonyesha wazi yaliomo ndani yake na yanamiliki picha za uchi na zile za ngono nyingi zikiwa za watoto.
Pia yana maoni ya ngono yanayochapishwa na wateja wake.
Pia kuna picha ambazo zimeibwa kutoka kwa mtandao wa facebook na magazeti ambazo zinaandamana na maoni machafu.
Kwa mfano Diana {sio jina lake} aligundua picha za mwanawe wa kike zimeibwa katika blogu yake.
Zilichapishwa katika mtandao unaotumiwa na watu wanaowatamani watoto kingono na zimekuwa zikisambazwa miongoni mwa wanachama wake ambao pia walichapisha maoni machafu kuzihusu
chanzo:bbcswahili

0 comments: