Mahakama kujadili mapenzi ya jinsia moja India

...................


 

Mapenzi ya jinsia moja
Mahakama ya India imekubali kusikiliza kesi ya kutaka kubatilisha sheria ya kikoloni ambayo ian haramisha mapenzi ya jinsia moja.
Swala hilo sasa limewasilishwa mbele ya mahakama ya majaji watano,hatua ambayo inaonekana kuwa muhimu miongoni mwa jamii ya wapenzi wa Jinsia moja na wanaharakati.
Wanaharakati nje ya mahakama ya juu nchini India walishangiliwa uamuzi huo, ambao umetaka sheria moja wapo tata zaidi nchini humo kufanyiwa marekebisho.
Chini ya sheria ya sasa ya India mapenzi ya jinsia moja ni hatia inayotoa adhabu ya kifungo cha jela.
Japo sheria hii haijakua ikitekelezwa, wapenzi wa jinsia moja wanasema imekua ikitumia kuwahangaisha.
Mwaka wa 2009, mahakama kuu mjini Delhi ilitupa nje sheria hiyo hatua iliyopongezwa na wengi.
Hata hivyo miaka minne baadaye Mahakama ya juu ikabatilisha uamuzi huo.
Hatua ya leo inafungua ukurasa mpya wa kutegua kitendawili cha sasa cha sheria nchini India.
Lakini kwa wengi ni hatua moja ambayo imewapa motisha wapenzi wa jinsia moja nchini humo

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: