Mkuu wa Mafia

...................

 
Mkuu wa zamani wa genge la Mafia amepigwa risasi na kuuwawa nchini Canada.
Mkuu wa zamani wa genge la Mafia amepigwa risasi na kuuwawa nchini Canada.
Rocco Zito, aliyekuwa na umri wa miaka 87, aliuwawa nyumbani mwake mjini Toronto Canada.
Mkwewe, (Domenico Scopelliti), ameshtakiwa kwa mauaji hayo, baada ya kujisalimisha kwa polisi.
Kwa miaka kadha, Rocco Zito alikuwa kati ya viongozi wa kundi la mafia, 'Ndrangheta', lenye asili ya Calabria, Italiana, na alikuwa akiongoza katika uhalifu nchini Canada.
Polisi wanasema kuwa waliwasili nyumbani kwa Zito na wakampata keshapigwa risasi.
Juhudi za kumuokoa hazikufua dafu.
Aliaga dunia kabla ya kufika hospitalini.
 
Zito alizaliwa mjini Fiumara, Calabria, Italy, mwaka wa 1928 alihamia Canada miaka ya 1950.
Zito alizaliwa mjini Fiumara, Calabria, Italy, mwaka wa 1928 alihamia Canada miaka ya 1950.
Alihusishwa na visa vya utovu wa usalama na magenge ya 'Ndrangheta New York, Montreal na Italia.
Polisi nchini Italia wanasema kuwa genge lake ndilo linalolangua mihadarati aina ya kokain barani Ulaya


chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: