WAKILI INDIA AMSHTAKI MUNGU
Wakili amshtaki mungu wa Kihindi India
Ram ni mmoja wa miungu wanaoabudiwa na kutukuzwa sana na Wahindi
Wakili mmoja nchini India ameshangaza wengi baada ya kuwasilisha kesi dhidi ya mungu anayetukuzwa sana na Wahindi kwa jina Ram.
Wakili huyo Chandan Kumar Singh anasema “Bwana Ram alimdhalilisha mkewe Sita".
Alitaka mahakama katika jimbo la Bihar, mashariki mwa India, ithibitishe hilo.
Ram ndiye huangaziwa kwenye Ramayana, utenzi wa beti 24,000 ulioandikwa kwa lugha ya Kisanskrit.
Huabudiwa na mamilioni ya watu India na kote duniani.
Bw Singh anaamini kwamba kesi yake ina msingi.
Ananukuu vitabu vya kidini kutetea hilo.
“Inajulikana
wazi kwamba Ram alimtaka Sita athibitishe kwamba bado alikuwa msafi
baada yake kumuokoa kutoka kwenye minyororo ya mfalme muovu Ravana.
Hakumuamini Sita," Bw Singh ameambia BBC.
Kesi yake ya kwanza ilitupwa na mahakama wiki iliyopita lakini anasema atawasilisha kesi nyingine.
"Jinsi
Ram alivyomchukulia Sita ni dhihirisho kwamba wanawake hawakuheshimiwa
hata zamani. Ninajua hili huenda likaonekana suala la kipumbavu, lakini
lazima tujadili tamaduni zetu za kidini. Nitawasilisha kesi upya kwa
sababu ninaamini kwamba Wahindi sharti wakubali kwamba Ram
alimdhalilisha Sita."
Bw Singh amepuuzilia mbali madai kwamba anajitafutia tu sifa.
Amesema
watu hawawezi kuendelea kujadili kuhusu kuheshimiwa kwa wanawake ilhali
inajulikana wazi kwamba miungu huyo anayeabudiwa na wengi hakumheshimu
mkewe.
Hatua yake imeshutumiwa vikali hata na wenzake.
Baadhi wametishia kumshtaki na wengine kuomba chama cha wanasheria nchini humo kumpokonya leseni ya uanasheria.
“Huwa
twawatazama Ram na Sita kwa pamoja na huwaabudu walivyo kwa pamoja.
Hakuna suala la kuamini kwamba Ram alimdhalilisha Sita,” Ranjan Kumar
Singh, mmoja wa wanaompinga anasema
chanzo:bbcswahili

0 comments: