ZUMA ALIVYOINGIA BURUNDI....NI NOMA
Zuma aingia Burundi na ulinzi mkali wa kijeshi
Ujumbe wa Umoja wa Afrika unaowajumuisha marais watano uko mjini
Bujumbura kwenye ziara ya siku mbili inayolenga kuumaliza mgogoro mkubwa
wa kisiasa unaoikumba Burundi.
Ujumbe huo unaongozwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiandamana
na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Haile Mariam Deseleyn, na marais wa Alli
Bongo Ondimba wa Gabon, Mohamed Ould Abdelaziz wa Mauritania na Macky
Sall wa Senegal.
Kilichowashangaza wengi mjini Bujumbura ni hatua ya Zuma kuwasili akilindwa na walinzi wake wapatao 50 kutoka nchini mwake wakiwa kwenye magari sita ya kijeshi.
Wakati huo huo, wapinzani waishio uhamishoni wameeleza kukasirishwa kwao na kauli ya Rais Pierre Nkurunziza kuwa hatazungumza na wale aliowaita "magaidi" anaowatuhumu kushiriki katika vitendo vya kuvuruga usalama.
Mazungumzo ya awali yalikwama baada ya serikali ya Burundi kukataa kukaa meza moja na wapinzani inaowahusisha na jaribio la kijeshi lililoshindwa mwezi Mei mwaka jana.
chanzo:dw swahili

0 comments: