PAPA ASEMA"UOGA UTAWAFANYA WAKRISTO WAFUNGWA"

...................
.
 Papa Francis : Uoga utawafanya Wakristu wafungwa

 .
  Papa Francis aongoza misa ya jumapili ya pasaka Roma

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anahudhuria misa ya Jumapili ya pasaka inayojumuisha maelfu ya wakatoliki.
Aliwabariki waumini waliohudhuria misa hiyo kwa baraka ya kitamaduni ya "urbi et orbi" na ile ya ''Miji na dunia nzima''.
Awali papa Francis aliwaomba wakristo kote duniani wasiruhusu uoga uwatawale.
Akizungumza katika mkesha wa sherehe za pasaka na wiki moja baada ya mashambulio ya Brussels yalliyowauwa watu 31 ,papa Francis amewataka waumini kutopoteza matumaini akisema hilo litawafanya wafungwa.
Wachambuzi wanasema swala la jinsi ya kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi ndilo litakalokuwa mada kuu ya ujumbe wa papa Francis Jumapili hii ya pasaka.
Mwandishi wa BBC aliyeko Roma anasema kuwa hotuba hiyo ilikuwa tofauti zaidi na ile aliyewakashifu waumini wa dini zingine wanaojaribu kudunisha dini zingine

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: