TAALUMA UNAZOTAKIWA KUSOMEA ILI ULIPWE ZAIDI HIZI HAPA
Je unataka kulipwa mshahara mkubwa ?Soma utafiti
Je unataka kulipwa mshahara mkubwa ?
Unahitaji kujifunza udaktari au maswala ya kiuchumi.Utafiti wa mafunzo ya fedha IFS umeripoti kuwa wanafunzi waliosomea utabibu na maswala ya kiuchumi huwa na mshahara mkubwa zaidi baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 10.
Wanaume wanaohitimu katika masomo hayo hujizolea takriban pauni elfu 55,utafiti huo umebaini.
Taaluma zenye faida kubwa | |
---|---|
Shahada | Mapato |
Udaktari | £ 55,000 |
Uchumi | £ 42,000 |
Uhandisi na Teknolojia | £ 31,200 |
Sheria | £ 30,100 |
Sayansi | £ 29,600 |
Elimu | £ 29,600 |
Usanifu mijengo | £ 28,600 |
Hisabati na Sayansi ya Kompyuta | £ 26,800 |
Biashara | £ 26,500 |
Sayansi ya Jamii | £ 26, 200 |
Historia na Falsafa | £ 26,500 |
Bayolojia | £ 25,200 |
Kilimo | £ 21,400 |
Habari na Mawasiliano | £ 19,300 |
Utafiti huu unatilia pondo dhana kuwa shahada
za sanaa na ubunifu hazilipi vyema ikilinganishwa na zile za sayansi ama
hata sheria.
Mwanafunzi aliyehitimu na shahada ya sanaa na ubunifu anapokea mshahara wa chini wa takriban pauni 14,500.
Vilevile Utafiti huu unasisitiza haja ya kwenda shule.
Mashirika na makampuni yanapendelea wafanyikazi waliohitimu japo na shahada moja kuliko wale ambao hawakufuzu katika vyuo vikuu.
Utafiti huu vilevile unathibitisha kuwa wanaume hulipwa zaidi ya wenzao wa kike katika kile sekta ya uchumi.
Bi
Anna Vignoles mmoja wa watafiti walioandika ripoti hii wanasema kuwa
hii ni fursa kwa manwafunzi yeyote yule achague vyema taaluma anayotaka
kujiunga nayo kwani uamuzi wake utakuwa na madhara ya kudumu katika
maisha yake ya usoni.
Utafiti huo umegundua kuwa watoto wa
matajiri wenyewe pia hupata senti nyingi na kufanikiwa maishani
ikilinganishwa na watoto wa masikini.
Hayo yalibainika baada ya
utafiti wa kina miongoni mwa wanafunzi 260,000 waliotuma maombi ya
ufadhili vyuoni kati ya mwaka wa 2003 hadi mwaka wa 2013.
chanzo:bbcswahili
0 comments: