WALALA KATIKA MAPIPA YA TAKA WAONGEZEKA
Wanaoishi katika mapipa ya taka UK waongezeka
Watu wanaoishi katika mapipa nchini Uingereza
Idadi ya watu wasio
na makao na ambao sasa wanaishi katika mapipa ya taka inaendelea
kuongezeka nchini Uingereza kulingana na kampuni kubwa ya kuzoa takataka
nchini humo.
Lakini ni kwa nini hili linatokea?''Katika barabara unatukanwa na hata kunyanyaswa.Usiku uliopita vijana wachache walikuwa wanatembea karibu yangu na mwengine akanipiga teke la uso.Lakini katika mapipa unaweza kujificha ili watu wasikuone.Kuna joto hakuna mtu anayejua ulipo,''George analezea kuhusu barabara ya Bristol.
Amekuwa bila makao tangu alipopoteza kazi yake ya uhandisi kabla ya krisimasi,na kumfanya kushindwa kulipa kodi ya nyumba.
Mnamo mwaka 2014 kampuni hiyo iligundua watu 31 waliokuwa wakilala katika mapipa tofauti ya takataka.
Mwaka mmoja baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 93 na mwaka huu ambao unaisha mwezi Machi, idadi hiyo imefikia 175 kufikia sasa
chanzo:bbcswahili

0 comments: