CUF WANYOKA NA Prof. Lipumba:SIKILIZA HAPA
Ikiwa
ni siku kadhaa tangu tamko la msajili wa vyama vya siasa kueleza
msimamo na ushauri kuhusu mgogoro unaoendelea kwenye chama cha wananchi
CUF, katika msimami uliotolewa na msajili wa vyama ulieleza kuwa Profesa
Ibrahim Lipumba ni mwenyekiti halali wa CUF vilevile wanachama
waliokuwa wamefukuzwa na kusimamishwa ni wanachama halali
Baada ya
tamko hilo Profesa Ibrahim Lipumba alifika katika ofisi za chama CUF
makao makuu jijini Dar es salaam akisindikizwa na wafuasi wake kwa ajili
ya kuanza rasmi shughuli za uenyekiti wa chama.
Leo
September 26, 2016 taarifa iliyotolewa na kituo cha ITV imeeleza kuwa
Baraza kuu la uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi CUF limefanya kikao
cha kujadili suala hilo na maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo ni
kumfukuza uanachama Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na makosa
mbalimbali ikiwemo kutumia vijana kuvunja ofisi za CUF na kuingia kwenye
ofisi hizochanzo: http://millardayo.com

0 comments: