MADREVA WA MALORI 12 WA TANZANIA WATEKWA KONGO
Baada
ya Taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utekwaji wa
madereva kutoka Tanzanjia huko Congo, Leo September 15 2016 taarifa
imetolewa na serikali kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa
Afrika Mashariki.
Taarifa
hiyo imesema kwamba Serikali imepokea juu ya kutekwa kwa malori 12
katika eneo la Namoyo jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo mnamo September 14, 2106. Taarifa imesema kuwa kati ya malori
hayo, nane yanamilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji na mengine
yanamilikiwa na wafanyabiashara Kenya.
Kwa mujibu
wa taarifa hiyo ni kwamba waliofanya utekaji ni kikundi cha waasi cha
MaiMai na baada ya utekaji magari hayo, waliwashusha madereva na
kuwapeleka porini kisha kuyateketeza kwa moto malori manne ambayo yote
ni ya Dewji.
Watekaji
hao walitoa saa 24 kuanzia kuanzia jioni ya September 14 wakitaka
walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili
waweze kuwaachia pia walitishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa
kiasi hicho cha fedha walichokitaka mpaka kufikia jioni ya September 15.
Taarifa za
awali zimedai kuwa madereva wawili kutoka Tanzania walifanikiwa
kutoroka na ndio waliotoa taarifa za kuhusu tukio hilo. Serikali kupitia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema
imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili
kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa haraka iwezekanavyo wakiwa
salama kabisa.

0 comments: