Mahakama ya juu Ufaransa kuamua kuhusu marufuku ya vazi la Burkini
Mahakama
ya juu nchini Ufaransa hii leo itaamua ikiwa ibatilishe uamuzi wa awali
wa mahakama kuu uliopiga marufuku vazi la kuogelea la Burkini, uamuzi
ambao ni wazi umesababisha sintofahamu sio tu Ufaransa lakini nje ya
nchi.
Mahakama hiyo itasikiliza
utetezi wa shirika la kutetea haki za binadamu pamoja na ule wa taasisi
inayopinga ubaguzi dhidi ya Uslamu, ambapo wanaomba kurejewa upya kwa
uamuzi uliotolewa kusini mwa mji wa Villeneuve-Loubet, ambako vazi hilo
la kiislamu la kuogelea lilipigwa marufuku.Uamuzi huu ambao unatarajiwa kutolewa majira ya saa tisa mchana kwa saa za Paris ambapo Afrika mashariki itakuwa ni saa kumi jioni, utatoa taswira rasmi ya karibu ya miji 30 ya Ufaransa ambayo ilitangaza kupiga marufuku vazi hilo ambalo muogeleaji wa kike hujifunika mwili mzima.
Mwanzoni mwa juma hili, mahakama ya eneo la utalii la Riviera mjini Nice, ilitoa uamuzi kuidhinisha marufuku ya vazi hilo.
Zuio la vazi la Burkini kwenye miji kadhaa nchini Ufaransa, limezua hali ya sintofahamu na mjadala mkali kuhusu vazi hilo linalovaliwa na wanawake wanapokuwa kwenye maeneo ya fukwe ambapo huwafunika mwili mzima, huku wanaharakati wa haki za binadamu wakihoji ziko wapi haki za wanawake?
Haya yanajiri wakati huu, watu wenye misimamo mikali kuhusu uislamu wakutaka mahakama ipige marufuku vazi hilo, kwa kile wanachosema hutumiwa na wanawake kuficha maovu yao na hata wakati mwingine kutumiwa na wanajihadi kujilipua
chanzo: http://sw.rfi.fr/ulaya/20160826-mahakama

0 comments: