Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amtukanaRais Wa Marekani
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amtukanaRais Wa Marekan ajutia maneno yake
Jumanne,
Septemba 6, Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameelezea masikitiko yake
baada ya kumkashifu Rais wa Marekani Barack Obama Jumatatu wiki hii
akimtaja kuwa ni "mwana wa kahaba."
Wakati
huo huo Barack Obama amefuta mkutano wake iliyokuwa umepangwa Jumanne
hii Septemba 6 na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte. Uamuzi huo unakuja
baada ya rais wa Ufilipino kumtusi hadharani mwenzake wa Marekani.
Mzozo
halisi wa kidiplomasia umeendelea kukua kati ya Marekani na mshirika
wake Ufilipino katika siku za hivi karibuni. Washington na Manila
wanashirikiana hasa katika makubaliano ya kijeshi.
Wakati wa
mkutano baina ya viongozi hawa wawili uliyokua umepangwa kufanyika
Jumanne hii katika mji wa Laos, Barack Obama alitaka kujadili na
mwenzake Duterte kuhusu ukandamizaji dhidi ya madawa ya kulevya
uliyosababisha, kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu, vifo vya
watu karibu 2 000 nchini Ufilipino, miongoni mwao watu wengi wasio na
hatia.
Rais Rodrigo Duterte, ambaye tayari anajulikana kwa kauli
zake mbovu, na sera zake zenye mashambulizi alijibu katika mazungumzo
hayo akimuita Obama "mwana wa kahaba."
Rais
wa Marekani, akihojiwa na waandishi wa habari, ameonekana kuchukua
mambo kifalsafa, akielezea kuwa Rais Duterte alikuwa mtu "mwenye
hasira", na angeweza kukutana kama angelikuwa na uhakika wa kukutana na
rais wa Ufilipino ili kuzungumzia mambo ya ujenzi wa nchi hizo mbili.
Msemaji
wa baraza la taifa la usalama Marekani Ned Price ameambia wanahabari
kwamba Bw Obama atakutana na Rais wa Korea ya Kusini Park Geun-hye

0 comments: