UNALIKUMBUKA SAKATA LA SNOWDEN NA SIRI ZA MAREKANI...? BASI Edward Snowden aomba Obama amsamehe

...................


mediaEdward Snowden katika mkutano na waandishi wa habari, Septemba 14, 2016.REUTERS/Brendan McDermid
Edward Snowden amemuomba Rais wa Marekani, Barack Obama, amsamehe kabla ya kumaliza muhula wake mwezi Januari 2017. Bw Snowden anaamini kwamba siri alizoziweka wazi zilisaidia nchi yake. Ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Uingereza la Guardian, Jumanne hii, Septemba 13.
"Ndiyo, kuna sheria zinazozungumzia mambo fulani, lakini labda ndio maana kwa utawala kutoa msamaha wake, lakini kuna mambo ya kipekee yasiyokua halali ambayo mantiki nyingine kiuadilifu au kimaadili yanaonekana kuwa yanahitajika na ni muhimu, " amesema Edward Snowden katika mahojiano ya video ya dakika chache yaliyorushwa na gazeti hilo la Uingereza.
"Nadhani wakati watu wanaangalia faida, ni wazi kwamba tangu mwaka 2013 sheria za nchi yetu zimemebadilika. Taasisi zote za uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na baraza la wawakilishi, vyombo vy sheria na rais, kila mtu amebadili sera yake baada kuweka wazi siri hizi. Wakati huo huo, hakukuwa na ushahidi wowote kwamba kuna mtu aliyeumizwa kwa siri nilizoweka wazi, " ameongeza mshauri wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa (NSA).
Mwezi Julai, Ikulu ya White Houseilipinga kupokea waraka uliyotolewa kwa kudai msamaha bila masharti kwa Snowden, ambaye mwaka 2013 aliweka wazi uzito wa mtandao wa upelelezi wa kielektroniki wa Marekani. Edward Snowden "anatakiwa kurudi Marekani kushitakiwa na wenzake na si kujificha nyuma ya utawala wa kimabavu. Kwa sasa, anakimbilia matokeo ya matendo yake ", amesema Lisa Monaco, mshauri wa Rais Barack Obama katika masuala ya Usalama wa Ndani mapoja na mapambano dhidi ya ugaidi.
Bw Snowden alishtakiwa kwa upelelezi nchini Marekani, baada ya kukimbilia nchini Russia. Anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela nchi mwake. Aliibai nyaraka nyingi za siri alipokua akihudumu katika Shirika la Usalama wa Taifa (NSA), moja ya mashirika ya siri ya upelelezi ya Marekani

chanzo: http://sw.rfi.fr
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: