ASKARI FEKI AKAMATWA MWANZA
Jeshi la polisi Mwanza limemkamata askari feki
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza
linamshikilia Ahmed Gabo umri wa 22 kwa tuhuma za kukutwa amevaa sare za
jeshi la Polisi kinyume na sheria, Gabo anadaiwa kuiba sare hizo, millardayo.com na Ayo TV imempata Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza, Ahmed Msangi na amezungumza haya………
‘Kwa
jinsi alivyovaa sare za Polisi kofia, mkanda mpaka viatu na hali
aliyokuwa nayo ni kinyume na askari anavyotakiwa awe na maadili
aliyokuwa anaonyesha sio ya Kipolisi’
‘Tumemhoji
kwa haraka na amekiri ni kweli hizi sare sio zake na wala hajawahi kuwa
kwenye mafunzo yeyote ya kijeshi bali ameiba begi la muumini ambae
alikuwa anaswali katika msikiti siku nne zilizopita huyu muumini ni
Askari Polisi wa hapa mkoani;-
Ahmed Msangi
Kumsikiliza kamanda Ahmed Msangi unaweza kubonyeza play hapa chini
chanzo:http://millardayo.com/akt52/

0 comments: