RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI HOSTELI ZA CHUO KIKUU CHA UDSM
Leo
October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka
huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya
chuo hicho.
Wakati
Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi
umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo
yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.
Rais Magufuli ameahidi kuwa, kwa kuwa
majengo hayo yanauwezo wa kubeba ghorofa sita, Serikali itafanya
utaratibu wa kutumia moja ya likizo za wanafunzi kuongeza ghorofa
nyingine mbili ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata nafasi.
Rais Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi
Rais Magufuli na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa
ufafanuzi kwa Rais Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli

0 comments: