AFUATA NYAYO ZA MESSI KUKWEPA KODI

Mamlaka nchini Hispania zimedai kuwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez alidanganya kuhusu mapato yake akiwa mchezaji wa Barcelona na kukwepa kulipa kodi. Kulingana na gazeti la El Periodico, waendesha mashtaka mjini Barcelona wamedai Mchile huyu mwenye umri wa miaka 27 hakulipia kodi ya mapato ya Dola million 1 za Marekani kati ya mwaka 2012 na 2013.
Gazeti hilo liliongeza kuwa Sanchez anadaiwa kuficha mapato yake yanayotokana na haki za picha kwa kutumia kampuni ya nchini Malta ijulikanayo kama Numidia Trading. Hata hivyo, wakala wake Fernando Felicevich amejitokeza kumtetea, akisema mteja wake ametii sheria zote za mataifa ambayo ameishi.
Lionel Messi, naye alihukumiwa kwenda jela miezi 21 kwa kukwepa kulipa
kodi na mahakama ya Barcelona mwezi Julai. Mbali na hapo Javier
Mascherano, mshambuliaji wa Barcelona, pia alihukumiwa mwaka mmoja jela
kwa kosa kama hilo mwezi Januari, wakati uchunguzi bado unaendelea kwa
Samuel Eto'o na Adriano.
chanzo: https://www.facebook.com/kiswahilicri/?hc_ref=NEWSFEED
chanzo: https://www.facebook.com/kiswahilicri/?hc_ref=NEWSFEED

0 comments: