KLAB YA SIMBA YATANGAZA MAREKEBISHO MADOGO KATIKA USAJILI

...................


Klabu ya Simba imetangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya katika dirisha dogo la usajili lililofungwa jana ambapo imewaacha rasmi Golikipa raia wa Ivory Coast Vicent Agban na kiungo kutoka Kongo Mussa Ndusha.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa vya vyombo vya habari imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog
Taarifa hiyo pia imethibitisha Simba kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, huku ikikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Luizio anayejiunga nayo kwa mkopo toka Zesco ya Zambia.
Katika maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu.
Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui FC ya Shinyanga, pamoja na Emmanuel Semwanza atakayekwenda Majimaji FC ya Songea,
Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Alli kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta ilikuwa imempeleka kwa mkopo.

chanzo: http://swahili.cri.cn/141/2016/12/16/1s159677.htm
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: