VIDEO: TAMKO LA SERIKALI JUU YA AJIRA MPYA ZA UALIMU
December 15 2016 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
alikutana Dodoma na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ili kujadili
namna sahihi ya kuboresha sekta hiyo katika kipindi cha awamu ya tano
ambapo katika baadhi ya vitu alivyogusia ni pamoja na suala la ajira kwa
walimu.
Waziri Ndalichako amesema…>>>’Utaratibu
wa kuajiri tunauboresha, zamani ilikuwa ukisoma ualimu unapangiwa
sehemu ya kazi bila hata kuhakikiwa lakini sasa ni lazima kila
anayemaliza mafunzo ahakikiwe kwanza ndipo hatua zingine zinafuatwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
‘Tumebaini kwamba serikali
imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwa kuajiri watu wasiokuwa na sifa,
tayari katibu mkuu wa wizara yangu ameshatoa tangazo kwa wahitimu wote
waliomaliza mafunzo ya sayansi mwaka 2015 wawasilishe vyeti vyao ili
vihakikiwe‘ –Pro. Joyce Ndalichako
‘Na
wale watakaoonekana wana vyeti visivyokuwa na mashaka ndio watakaopata
nafasi kwahiyo zoezi la ajira kwa walimu limeanza hivyo tunaamini tatizo
la ajira kwa walimu haliakwisha lakini tutakuwa tumelipunguza kwa
nafasi kubwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
unaweza kuendelea kumsikiliza Pro. Joyce Ndalichako kwenye hii video hapa chini…
chanzo:milardayo.com
0 comments: