Ujerumani kununua ndege zisizo na rubani.
Ujerumani inao mpango wa kununua ndege 16 zisizoendeshwa na rubani mnamo kipindi cha miaka michache ijayo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa gazeti liitwalo Spiegel. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuahirishwa mpango wa kutengeneza ndege za aina hiyo ambazo zingejulikana kama Euro Hawk.
Waziri wa ulinzi Thomas de Maiziere tano kati ya ndege hizo zitakazonunuliwa zitakuwa kazini ifikapo mwaka 2016. Kulingana na ripoti ya gazeti la Spiegel, tayari Marekani imekwisharidhia mauzo ya ndege hizo.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa waziri de Maiziere amesema kuwa Ujerumani itakuwa na haki ya kuweka silaha katika ndege hizo. Mpango wa ununuzi wa ndege hizo zisizo na rubani unatarajiwa kupitishwa na serikali ya Kansela Angela Merkel katika mkutano wa baraza la mawaziri leo hii.
chanzo:Dw swahili
0 comments: