199 wafariki kutokana na moto China
Maafisa wa Serikali kutoka
Kaskazini Mashariki mwa Uchina wamesema kuwa moto mkubwa uliotokea
katika kiwanda cha kuchinja Kuku umewaua watu 119 baada ya watu hao
kukwama katika vyumba vya kiwanda hicho kilichokuwa kinaungua.
Watu zaidi ya hamsini
wamejeruhiwa.Haijathibitika kama gesi ya mbolea ya aina ya Ammonia
ilivuja au nyaya za umeme ndizo zilizosababisha moto huo katika mji wa
Mishazi. Waokoaji wangali wanaendelea na shughuli za uokozi.Watu wanaoishi katika eneo la kilomita moja kutoka kiwanda hicho wamehamishwa.
Kwa kawaida viwango vya usalama katika maeneo ya kazi nchini Uchina ni vya hali ya chini. Vifo vimeripotiwa mara kwa mara katika viwanda na machimbo nchini humo.
Shirika rasmi la habari nchini humo Xinhua limesema watu 100 waliweka kukimbilia usalama wao kutoka kwa kiwanda hizho ambacho lango lake kuu lilikuwa limefungwa wakati moto huo ulipozuka. Liliongeza kwamba shughuli ya uokozi ilikuwa ngumu kutokana na muundo wa jengo hilo.
Na bbcswahili
0 comments: