Mafuriko makubwa yashuhudiwa Ulaya
Maelfu ya watu wametoroka makaazi yao katika sehemu nyingi za Ulaya kufuatia mafuriko mabaya katika maeneo hayo.
Shughuli za dharura za uokozi, zinaendelea
nchini , Austria, Ujerumani na Jamuhuri ya Czech kukabiliana na mafuriko
makubwa kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo.Nchini Ujerumani, zaidi ya watu 7,000 wamehamishwa kutoka makwao mjini Eilenburg.
Wakaazi wa mji mkuu wa Check, Prague, wanajiandaa kwa kile kinachosemekana kuwa mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini humo huku mto wa Vltava ukisemekana kuwa karibu kuvunja kingo zake kufuatia mvua kubwa ya siku kadhaa.
Wafanyakazi wa kukabiliana na hali ya hatari wameweka vizuizi vya vyuma na magunia ya changarawe, ili kujaribu kukinga mji huo kutokana na mafuriko hayo.
Mji huo unatarajiwa kuvunja kingo zake wakati wo wote sasa.
Mnamo Jumapili, Serikali ya Check ilitangaza Hali ya Hatari kote nchini.
Maeneo mengine tayari yamefurika maji. Serikali katika mataifa mengine katikati mwa Bara la Ulaya wako katika hali ya tahadhari kutokana na mvua kubwa inayonyesha. Mataifa hayo yanaandaa vizuizi kujihami dhidi ya mafuriko.
Kiwango cha maji katika Mto Rhine, Danube na katika vijito vingine vinavyoungana nao kinazidi kupanda. Hadi kufikia sasa watu watatu wamefariki kutokana na mafuriko katika eneo hilo.
Na bbcswahili
0 comments: