Rais Kikwete akabidhiwa rasimu ya katiba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na
tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika
katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia
mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania
kuhusiana na katiba wanayoitaka.Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapya.
Ameyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasimu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake. Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.
Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja.
Hata hivyo ripoti hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania Bara.
chanzo:bbcswahili

0 comments: