REKODI YAVUNJWA.....MKE WA KENYATTA AWEKA HISTORIA LONDON
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akimlaki mkewe Margaret baada ya kumaliza mbio za London Marathon kwa kutumia muda wa saa 7 na dakika nne.
Mama Margaret Kenyatta mke wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amekuwa mwanamke wa kwanza mama wa taifa kushiriki mbio za London Marathon na kumaliza mbio hizo.
Alishangiliwa
na wakenya wanaoishi nchini Uingereza alipomaliza mbio hizo za kilomita
42 kwa muda wa saa saba na dakika nne siku ya Jumapili.
Bi Kenyatta alishiriki mbio za London Marathon kama
sehemu ya mradi wake wa kuchangisha pesa za kuwasaidia wanawake
wajawazito kujifungua katika mazingira salama na kuhakikisha kuwa watoto
wao pia wanaishi nchini Kenya.Mama Margaret alilakiwa
na Rais Kenyatta pamoja na waandalizi wa mbio hizo mjini London
mwishoni mwa mbio huku akiwapa motisha wakenya na jamii ya kimataifa kwa
kuwa mke wa kwanza wa rais kuwahi kushiriki mbio hizo.
Lengo lake kuu ni kupunguza idadi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Wanawake
wengi na watoto wachanga nchini Kenya hupoteza maisha yao wakati wa
kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma salama na sasa mama Kenyatta
amejitwika jukumu la kuwapa akina mama wajawazito uwezo wa kujifungua
salama.
Bi Kenyatta alikuwa na kikundi cha wasaidizi 8 waliokuwa naye hadi alipofika mwishoni mwa mbio hizo.
Wakenya kutoka sehemu mbali mbali uingereza walifika mjini London kushuhudia Bi Kenyatta akikamilisha mbio hizo.
Wakenya ndio walioshinda mbio hizo upande wa wanawake na wanaume.
Wilson Kipsang aling'aa upande wa wanaume kwa kuweka rekodi mpya ya saa mbili na dakika nne. Kipsang alifuatiwa na mkenya mwenzakeStanley Biwott.
Kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat alishikilia nafasi ya kwanza akifuatiwa na mkenya mwenzake Florence Kiplagatchanzo brother danny blog

0 comments: