Okwi na Banda watokeo mara mbili usajili TFF.
Majina ya wachezaji Emmanuel Okwi na Abdi Banda yametokea kwenye timu mbili
SHIRIKISHO la soka Tanzania TFF,limetoa majina ya wachezaji wa timu
14 ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara huku majina ya wachezaji
Emmanuel Okwi na Abdi Banda yakitokea kwenye timu mbili Goal inafahamu.Goal imefika kwenye ofisi za TFF,na kujionea usajili huo mpya kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaotarajia kuanza Septemba 20,lakini jina la Okwi,likitokea kwa Simba na Yanga ilahali jina la Banda likitokea kwa timu za Simba na Coastal Union.
Goal iliwatafuta viongozi wa TFF wanaohusika na maswala ya usajili ili kujua mustakabali wa wachezaji hao lakini hawakuweza kupatikana na kulazimika kusubiri hadi siku ya mwisho ambapo Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji itakapokutana Septeba 6 ili kujadili mustakabali wa nyota hao
chanzo:goal.com

0 comments: