TUNDUMA HALI SI SHWARIIIIIIIIIII. KINAWEZA KULIPUKA LEO
Kumekuwa na hali ya sinto fahamu ndani ya mji wa Tunduma kufuatia raia kutaka kuandamana kwa kile wanachodai "kazi ya polisi ni nini"
Raia wamejawa na hasira baada ya kushuhudia matukio makubwa ya uharifu wa uporaji wa kutumia silaha katika mji wa Tunduma ndani ya wiki moja. matukio hayo ni pamoja na kuvamiwa kwa hoteli ya mzee Jomba,ambapo mzee Jomba alijeruhiwa na sasa yupo hospitali kwa matibabu.Usiku wa kuamkia leo sheli ya mnyonge nayo imevamiwa na waporaji hao na tukio jingine limefanyika mtaa wa sogea.
Raia hawaelewi kwanini kuna uharifu wakati polisi wapo? na hadi leo hakuna taarifa yeyote ile kutoka jeshi la polisi kituo cha Tunduma kwa raia juu ya uharifu huo.
Picha hapa chini zinaonyesha mji ulivyo siku ya leo.Hakuna mishemishe kabisaaaaaaaaaaa
ENEO LA AFRICANA HALI ILIVYO
MANZESE HAKUNA WATU
HATA ENEO MASHUHURI LA KWA JINA LA KISIMANI PAKAVU
TAARIFA ZAIDI ..............Endelea kuwa nasi

0 comments: