Wema ampongeza Diamond, amuita ‘kaka’,
Habari hiyo imekuja katika siku ambayp Diamond amegeuka shujaa kwa
kunyakua tuzo za tatu za Channel O. Miongoni mwa watu waliompongeza kwa
ushindi huo ni Wema Sepetu ambaye tumezoea akimuita staa huyo ‘my
baby’, awamu hii ameitwa ‘kaka’.
“Gnyt Instagramers… And Hongera tele ziende kwa kaka platnumz… I must
say he did Tanzania proud,” aliandika Wema kwenye Instagram muda mfupi
baada ya tuzo hizo kuisha ikimaanisha kuwa alikuwa akizifuatilia.
Tofauti na kwenye tuzo za MTV MAMA, msichana aliyekuwa ubavuni mwa
Diamond kwenye tuzo hizo ni Zari the BossLady – na hivyo kuthibitisha
tetesi zilizovuma kuwa wawili hao ni wapenzi.
Pamoja na Zari, Diamond alisindikizwa na mama yake ambapo walikuwa
pamoja na Zari kwenye red carpet na hata kuzunguka pamoja jijini
Johannesburg.
chanzo kengeteblog


0 comments: