WAPINZANI WA YANGU KUTUA TZ USIKU WA MANANE
Wapinzani wa Yanga timu ya Etoile du
Sahel kutoka Tunisia wanatarajiwa kuwasili saa 9 usiku kuamkia Ijumaa
kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na
msafara wa watu 56.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini Tunisia (FTF), Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa
na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Charefeddine Ridha, wachezaji
19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama
10
Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza
zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na Ijumaa wanatarajiwa kufanya
mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini
Msumbuji na walitarajiwa kuwasili mchana wa Alhamisi, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea
nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.
chanzo:bbcswahili
0 comments: